Haijachongwa kwenye marumaru.
Haijaandikwa kwa kuchorwa kwenye mbao.
Prem Rawat: Sanaa Kuu Kuliko Sanaa Zote
Haijachongwa kwenye marumaru.
Haijaandikwa kwa kuchorwa kwenye mbao.
Hapana.
Ni fursa kwa kila moyo utakaoguswa na zawadi ya Maarifa hayo, kwa wakati wake mwafaka.
Kupitia kwa mtu aliye hai.
(Hilo ni badiliko, sivyo?)
Mtu aliye hai.
Sisemi "mwanaume" au "mwanamke".
Mtu aliye hai ... atakuja na kutoa kipawa cha Maarifa kwa wale wanaokitafuta.
Mtu huyo ataweka masharti yake mwenyewe — na ndivyo itakavyokuwa daima — hakuna desturi ya kushikilia masharti yale yale. Masharti yatabadilika.
Mazingira yatabadilika, na kile kinachofaa kitatokea.
Mradi tu moyo umeguswa, basi inatosha.
Kutoka mahali hapo pa ndani ya moyo — na kugusa moyo wa mtu mwingine.
Hiyo ndiyo sanaa kuu kuliko sanaa zote.
Lakini ili kugusa moyo, inahitaji kutokuwa na hatia kwa mtoto na hekima ya maandiko yote matakatifu yakiunganishwa.
Kuishinda mipaka ya wakati, kumgusa mtu, kuzungumza na mtu.
Kuzungumza na watu elfu moja, na bado kuzungumza na kila mmoja kati ya hao elfu moja.
Hili si blanketi la plastiki.
Hili limesukwa kwa ustadi na kwa umakini, na limesukwa kwa ukamilifu.
Ni maneno ambayo, yanapougusa moyo, hutoweka.
Hayana tena umuhimu.
Tofauti kubwa sana.
Ni hitaji la msingi sana na la kweli kwa kila mwanadamu.
Lugha si muhimu.
Utamaduni si muhimu.
Mtu ni nani, yuko wapi, au si nani: hayo si muhimu.
Haya ndiyo mapokeo ya Maarifa: kuguswa moyoni.
Yafanye kuwa mapokeo yako.