Prem Rawat

Safari Takatifu Kuliko Zote

Kwa sasa, kwetu sisi,
kwa kila mwanadamu mmoja mmoja;
kila pumzi, kila wakati
ni ishara kwako
kwamba fursa yako ipo hapa.

Unapopumua, usifikirie kwamba ni "hewa",
bali ifikirie kama zawadi kuu kuliko zote
ambayo mwanadamu anaweza kupewa.

Elewa furaha,
furaha ya kuwa hai.

Na uelewe furaha,
furaha ya kuridhika kwa kuwa hai.

Elewa, pokea kwa unyenyekevu,
si kama haki yako — bali kwa unyenyekevu,
kwa moyo wa unyenyekevu,
kila pumzi inayoingia ndani yako.

Shukuru;
moyo huu uwe na shukrani.
Anza, katika maisha haya,
kuelewa maana ya kuwa hai.

Hii ndiyo safari takatifu kuliko zote utakayowahi kuifanya.

Hii ndiyo safari yenyewe.

Na mahali patakatifu kuliko pote ni wapi?

Ndani yako.