Sikiliza Moyo

Siku moja, wewe huyu hautakuwepo tena.

Hilo ni jambo la hakika.

Unajidanganya nani?

HAUTAKUWEPO tena. Mimi pia sitakuwepo. Ndivyo ilivyo. Ndivyo ilivyokuwa. Na kitakachokuwa je? Hakuna ajuaye.

Kama wasemavyo, "mavumbi hurudi mavumbini." Imesemwa vyema! Ndiyo, mavumbi hurudi mavumbini.

"Majivu hurudi majivuni." Hivyo ndivyo itakavyokuwa. Hilo ni jambo la kutarajia. Ni hakika kabisa.

Na sasa una nini?

Una uhai.

Tendo hilo rahisi tu la kuvuta pumzi moja baada ya nyingine. Je, unajua maana yake? Umewahi kuketi chini na kuelewa jambo hilo? Umewahi kuketi chini na kulihisi kweli?

Ukisubiri mpaka unapohangaika kuvuta pumzi, huwa umechelewa kidogo. Nimeona hilo pia: watu wakiwa wamelala hapo, wakijitahidi kuvuta pumzi. Wakati huo ndipo wanapotambua, ndipo wanapotambua jinsi kila kitu kilivyo muhimu.

Kama mtu angewaendea wakati huo, wanapojitahidi kuvuta pumzi, na kuwauliza, "Naweza kuazima gari lako?" Jibu lingekuwa, "Hebu! UNAWEZA KUCHUKUA!"

"Lakini unajua huwezi kufa sasa hivi; huwezi kuacha kupumua sasa hivi kwa sababu una mkutano na mawakili wako baada ya dakika 15."

Haijalishi. "Waambie nimewasalimu... kwaheri."

Jambo fulani huwa wazi kabisa — kwa dakika moja. Lakini si lazima iwe hivyo. Uwazi huo unaweza kuwa sehemu ya maisha yako sasa hivi.

Haya si "maneno tu".

Ninachowapa watu ni njia ya kuweza kujielekeza ndani yao wenyewe. Kama vile kioo, kinachokuwezesha kujitazama ndani yako.

Watu husema, "sawa, kwa nini ninahitaji hilo?"

Angalia, una macho mazuri sana; unaweza kuona kila kitu. Lakini kuna kitu kimoja ambacho macho yako hayawezi kuona: uso wako mwenyewe.

Unaweza kuona mikono yako, unaweza kuona viatu vyako, lakini kuna kitu kimoja ambacho macho yako hayawezi kuona: uso wako mwenyewe. Kwa hilo unahitaji kioo.

Hicho ndicho ninachowapa: njia ya kuingia ndani yako na kufurahia uzuri uliomo ndani yako.

Mimi siumbii uzuri huo. Si jambo la mawazo tu.

Hautokani na kitabu; hautokani na mawazo ya watu. Ni kitu kilicho ndani yako.

Na ninachowaambia watu ni: njoni msikilize. Na tafakarini kuhusu jambo hili.

Msifanye haraka — tafakarini. Mkiwa na maswali, yaulizeni.

Lipimeni, lichunguzeni, lihisieni. Na kisha — mtakapokuwa tayari — mtakuwa nalo.

Huo ndio mchakato. Rahisi sana na mzuri sana.

Na hicho ndicho ninachowapa watu.

Ikiwa mnapendezwa, mnaweza kuwasiliana nasi, kupata maelezo zaidi — njoni, msikilize.

Na kama hamna nia — hakuna shida.

Hazina hiyo bado itakuwa ndani yenu.

Uzuri huo utakuwa ndani yenu DAIMA.

Kama hamna nia, hakuna shida, lakini kumbukeni tu — kwamba mmejaliwa; kwamba muujiza wa ajabu sana umetokea.

Na muujiza huo si mti unaomea kutoka kwenye mwamba... bali muujiza huo ni NINYI.

Ninyi ndio muujiza.

Na ikiwa kwa namna fulani mnaweza kuufungua moyo wenu, kuuelewa na kuuhisi, kisha kuanza kusoma maneno yake moja baada ya jingine katika kitabu hicho cha mioyo, basi ninyi ndio mtakaofaidika na kitabu hicho.