Prem Rawat akizungumza

Maisha hucheza na kujidhihirisha kila siku
kwa njia rahisi na tulivu kabisa.

Upo, si kwa kupitia njia za ulimwengu huu, bali kwa jinsi ulivyo tu.

Ni wewe tu—uso huu, tabasamu hili, mwili huu, pumzi hii, moyo huu.

Watu wengi huzingatia matatizo yote yaliyopo duniani
na kusema kwamba tunapaswa kutafuta suluhisho la matatizo hayo yote.

Mimi nasema kwamba tuna safari ya kutafuta.

Si safari iliyoanzishwa na wewe au mimi.
Ni safari ambayo tayari ilianza kwa ajili yetu.

Ni safari ya kutafuta amani, safari ya kutafuta upendo,
safari ya kutafuta kuelewana, na safari ya kutafuta furaha.

Safari hii si ya kutafuta
furaha inayopatikana nje yetu.

Ni ya kutafuta furaha inayopatikana ndani yetu.
Safari hii si ya kutafuta amani iliyo nje yetu,
bali amani iliyo ndani.

Habari njema ni kwamba kile unachokitafuta, tayari unacho.

Mwonekano wa hadhira wakati wa hotuba ya Prem Rawat

Nani ametutambulisha sisi kwetu wenyewe?

Kila mara tunatambulishwa kwa mtu mwingine.
Hakuna anayetuuliza, "Hivi, umewahi kukutana na wewe mwenyewe?"

Kukutana na wewe mwenyewe ndiko kunakotofautisha kuwa huru na kukwama.
Usipotaka kukutana na wewe mwenyewe, unabaki umekwama na wewe mwenyewe.

Siku unapotaka kukutana na wewe mwenyewe, unakuwa huru.

Nitawaambia kuhusu
kitabu bora zaidi kuwahi kuandikwa.

Ni kitabu cha mawazo unayoyaandika kwa ajili yako mwenyewe. Kiko wazi.
Hakihitaji utangulizi; hakihitaji dibaji.
Hakihitaji maelezo ya chini ya ukurasa. Ni chako.

Ni shairi linaloimba moyoni mwako na kuamsha furaha.

Hilo ndilo shairi kuu kuliko yote—furaha.
Na ni shairi lako, namna ya kujieleza wewe mwenyewe.
Hiyo ndiyo zawadi kuu kuliko zote.

Ulimwengu huu umejaa maswali yasiyo na majibu.
Moyo huu umejaa majibu yasiyo na maswali.

Tunaweza kuyakubali hayo majibu, si yale ambayo ulimwengu unajaribu kutupatia.

Majibu ya moyo ni tofauti kabisa, kwa sababu moyo husema,

"Amka na ufurahi.
Amka uwe hai.
Amka uone uwezekano wa kupata utimilifu."

Prem Rawat jukwaani